1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Syria yaadhimisha mwaka mmoja tangu Assad alipoangushwa

8 Desemba 2025

Syria Jumatatu inaadhimisha mwaka mmoja tangu kuangushwa kwa mtawala wa kidikteta Bashar al Assad, wakati taifa hilo lililoganwanyika likapambana kurejesha utulivu na kujijenga upya baada ya vita vya muda mrefu.

https://p.dw.com/p/54w0U
Syria Damascus 2025 |Maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanguka kwa Assad | Rais Ahmad al-Sharaa katika Msikiti wa Umayyad
Rais wa Syria Ahmad al-Sharaa akizungumza baada ya kusali sala ya alfajiri katika Msikiti wa Umayyad katika kumbukumbu ya kwanza ya kuanguka kwa Bashar al-AssadPicha: Syrian Presidency/Handout/Anadolu/picture alliance

Rais wa mpito Ahmed al-Sharaa aliyefanikiwa kuongoza harakati za mapinduzi na kuuhitimisha utawala wa Bashar ameongoza maadhimisho hayo kwa sala ya alfajiri katika msikiti wa Umayyad, mjini Damascus, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la SANA.

Assad alikimbilia Urusi mwaka uliopita kufuatia mapinduzi hayo ambayo pia yalihitimisha vita vya zaidi ya miaka 13 vilivyotokana na uasi dhidi yake.

Kulingana na SANA, Sharaa, kamanda wa zamani wa kundi la kigaidi la al-Qaeda ameahidi kuijenga Syria tena ya haki na imara na miundo itakayoendana na nyakati za sasa na zilizopita.