Synodi yamalizika na atakaefuata Nyayo za Wowereit Berlin | Magazetini | DW | 20.10.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Synodi yamalizika na atakaefuata Nyayo za Wowereit Berlin

Mkutano wa wakuu wa kanisa katoliki wamalizika Vatikan bila ya maridhiano,na kuchaguliwa Michael Müller kumrithi Klaus Wowereit katika jiji la Berlin ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa magazetini

Synode ya familia huko Vatikan

Synode ya familia huko Vatikan

Tunaanza lakini na mkutano muhimu wa wakuu wa kanisa katoliki uliolengwa kufungua njia ya kuufanyia marekebisho mwongozo wa kanisa katoliki ulimwenguni.Waliotarajia watu walioachana watatambuliwa na kanisa katoliki wameula na chua linaandika gazeti la "Neue Westfälische" la mjini Bielefeld:"Kauli ya mwisho haijapitishwa katika mkutano huo muhimu wa wakuu wa kanisa katoliki-au Synode.Kanisa halikubadilisha kanuni na mwongozo wake-madhambi ni madhambi tu na ubora wa ndoa kati ya mwanamke na mwanamme haugusiki.Maaskofu hawana uwezo wa kubadilisha mafundisho ya dini ya kikristo.Suala tete lililougubika mkutano wa wakuu wa kanisa kama watu walioachana na kuwaowa au kuolewa na wengine waruhusiwe kujiunga na ushirika wa kidini bado halijajibiwa.Wakuu wa kidini waliohudhuria mkutano huo wa Vatikan wanaweza tu kutoa mapendekezo na kuelezea maoni yao.Wametoa lakini mwelekeo ambao hautapita vivi hivi.

Gazeti la Badische Neueste Nachrichten linamlinganisha Papa Fransis na kiongozi wa zamani wa kanisa katoliki Papa Paulo wa sita aliye aliyeliongoza kanisa katoliki hadi mwaka 1978 .Na huyo pia alitaka marekebisho yanayoambatana na wakati kwa upande mmoja lakini kwa upande wa pili alipiga marufuku matumizi ya vidonge vya kuzuwia uzazi.Gazeti linaandika:"Paul wa sita alifanya makusudi kupanda farasi wawili.Kwa namna hiyo alisababisha asipendwe na pande zore mbili.Wanaofuata muongozo asilia wanamkosoa wanasema anapigania sana maendeleo;kwa mfano pale alipovuwa taji lake-Tiara na kuamuru liuzwe ili fedha zilizopatikana ziwahudumie wasiojimudu.Wapenda mageuzi lakini wakimlinganisha na mtu wa zamani anaechukua tahadhari kubwa anapotoa maoni yake.BIla ya shaka Paul wa sita ametambua kwamba kanisa linabidi lijiambatanishe na wakati.Lakini mtu hawezi kumlinganisha na Papa Fransis.Hata Papa huyu wa sasa anaetokea Argentina anafanya tahadhari,kwasbabu anatambua yeye ni wa madhehebu ya Jesuit-hata hivyo lakini ni jasiri kuliko Paul wa sita.

Müller kufuata Nyayo za Wowereit Berlin

Mada yetu ya pili magazetini inahusu kinyang'anyiro cha kuania wadhifa wa meya wa jiji la Berlin.Wagombea watatu wa chama cha Social Democratic,akiwemo Raed Saleh,mjerumani mwenye asili ya Palastina walipigania wadhifa huo.Hatimae aliyeibuka na ushindi hakuna aliyemfikiria linaandika gazeti la "Lausitzer Rundschau":Hata Klaus Wowereit hakuwa akijulikana alipokabidhiwa wadhifa wa meya ya Berlin miaka 13 iliyopita.Hivi sasa amegeuka kuwa mwanasiasa aliyeongoza kwa muda mrefu zaidi serikali ya jimbo.Wowereit ndie chanzo cha kugeuka Berlin kuwa jiji la kusisimua na la kimataifa.Nyayo zake ni kubwa kwa hivyo Müller atabidi azifuate.Anatajikana kuwa mchapa kazi madhubuti na mwaminifu na hilo pekee linatoa matumaini

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Josephat Charo