Sydney, Australia. Polisi wapewa muda zaidi wa kuhoji. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Sydney, Australia. Polisi wapewa muda zaidi wa kuhoji.

Mahakama nchini Australia imewapa polisi muda wa nyongeza wa saa 48 ili kumhoji daktari mmoja raia wa India ambaye anashikiliwa kwa madai ya kuhusika na shambulio lililoshindwa la mwezi uliopita nchini Uingereza.Mohammed Haneef anaaminika kuwa anahusika na watuhumiwa ambao wanashikiliwa nchini Uingereza kuhusiana na shambulio dhidi ya uwanja wa ndege wa Glasgow.

Haneef alikamatwa wakati akijaribu kuondoka nchini Australia akiwa na tiketi ya kwenda India.

Familia yake nchini India imesema kuwa hana hatia na alikuwa tu anapanga kumtembelea mke wake na mtoto wao wa kike mchanga.

Polisi hivi sasa wanachunguza nyaraka 30,000 zilizokamatwa wakati wa msako katika majimbo matatu, ikiwa ni pamoja na mafaili katika laptop ya Haneef. Madaktari wengine watano kutoka India waliohojiwa nchini Australia kuhusiana na tuhuma za kuhusika na mpango huo unaohusishwa na kundi la kigaidi la al-Qaeda wameachiliwa huru.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com