Swali la Dafur Umoja wa Mataifa | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Swali la Dafur Umoja wa Mataifa

Dafur itakuwa mada ya mkutano wa siku 1 katika UM hii leo. Katibu mkuu Ban Ki-moon amesema UM utakua macho kuona Sudan inatekeleza ahadi zake za kurahisisha misaada kwa wakimbizi wa Dafur.

Katika mkesha wa majadiliano huko Umoja wa Mataifa, mjini New York, juu ya mzozo wa Dafur,mshtaki mkuu wa Mahkama kuu ya kimataifa inayohusika na uhalifu, amewataka viongozi wa dunia kukomesha kimya chao na kuweka usoni kabisa haki mbele ya ajenda ya mazungumzo yao. kwenye ajenda yao haki.

Nae Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amesema UM utakuwa macho kuona Sudan inatekeleza madai ya Baraza la Usalama kuwa iruhusu misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Dafur.

Akizungumza na kituo cha Tv cha CNN,katibu mkuu wa UM Ban Ki-Moon amesema amehakikishiwa na Rais Oumar Al Bashir wa Sudan kwamba misaada kwa mamilioni ya watu wanaoteseka na maafa huko Dafur,itawasili bila ya shida.

“Atatekeleza kwa uaminifu maazimio yote ya baraza la usalama la UM na jukumu iliobebea binafsi serikali yake.”Ban alisema.

Akaongeza kusema kwamba UM utakodoa macho kumtaka afanye hivyo na tutakagua utekelezaji wake.

Katibu mkuu wa UM alisema kwamba kupelekwa Dafur kwa kikosi cha pamoja kati ya UM na Umoja wa Afrika kumepiga hatua kubwa.

Mazungumzo hayo na kituo cha CNN,yamefanyika huku katibu mkuu akijiandaa kwa mkutano na rais wa Tume ya UA Alpha Oumar Konare hii leo utakowajumuisha wale wote wanaohusika na mgogoro wa Dafur.Kikao hiki cha siku moja kinalenga kukomesha umwagaji damu wa zaidi ya miaka 4 hukp Dafur,jimbo la magharibi la Sudan.

Kikao cha leo pia kitachimba msingi wa mazungumzo kati ya serikali ya Khartoum na waasi wa Dafur mjini Tripoli,Libya hapo oktoba 27.

Ufaransa jana imeitisha kuwapo kikosi cha pamoja cha kuhifadhi amani kati ya Umoja wa ulaya na Umoja wa Mataifa ili kuwalinda raia katika sehemu za Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako mzozo wa wakimbizi unaotokana na

Kikosi hicho kitajumuisha askari polisi 300 wa UM kikibeba jukumu la kutoa mafunzo kwa wachadi 850 ili washike zamu katika kambi za wakimbizi.Kikosi cha wanajeshi cha Umoja wa Ulaya cha hadi askari 4,000 kitakuwa na jukumu

la kulinda sehemu hizo.

Hili ni pendekezo lililo idhinishwa kimsingi na Umoja wa Ulaya hapo Julai,mwaka huu.Wanajeshi hao pia watakisaidia kikosi cha askari 26,000 cha UM na Umoja wa Afrika kinachotazamiwa kuanza kazi kikamilifu huko Dafur, hadi ifikapo kati ya mwaka ujao 2008.

Mshtaki mkuu wa Mahkama ya kimataifa juu ya uhalifu ametaka mada ya kuwahukumu wale waliohusika na kuuwawa kwa hadi watu laki 2 na kuwatimua maskani mwao wengine milioni 2.5 huko Dafur iwekwe mbele kabisa katika ajenda ya mazungumzo ya leo huko New York.

Mshtaki mkuu Luis Moreno-Ocampo mkutano huu utumiwe kuizindua serikali ya Sudan juu ya jukumu lake kumtia nguvuni waziri wake wa maswali ya kibinadamu,Ahmed Harun anaekabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa vita na dhidi ya ubinadamu.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com