SUVA : Mazungumzo yafanyika kuepusha mapinduzi | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SUVA : Mazungumzo yafanyika kuepusha mapinduzi

W aziri Mkuu wa Fiji na mjumbe wa kijeshi wamekuwa na mazungumzo kwa nyakati tafauti na Makamo wa Rais leo hii waktia juhudi zikiendelea kuepeusha mapinduzi yanayostishiwa kufanywa na mkuu wa majeshi wa kisiwa hicho.

Capteni Ben Nalva msaidizi binafsi wa mkuu wa majeshi Vorege Bainimarama alimtembelea Makao wa Rais kwa dakika 40 na baadae Waziri Mkuu Laisenia Qarase alijitokeza kutoka mafichoni na kuingia kwenye nyumba ya Makamo wa Rais ambako alibaki ndani kwa dakika 20.Akizungumza na waandishi wa habari baadae Qarase amesema kwamba mazungumzo yataendelea kati yao lakini hakutowa ufafanuzi zaidi juu ya mkutano wao.

Mikutano hiyo inaleta matumanini kwamba bado kuna nafasi ya kufanyika kwa mazungumzo kati ya pande mbili licha ya muda wa mwisho hapo Jumatatu uliowekwa na Mkuu wa majeshi wa Fiji Vorege Bainimarama kuitaka serikali itimize masharti kadhaa ya kujisafisha venginevyo ataipinduwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com