1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sura mpya ya utalii Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo

27 Agosti 2015

Watalii wachache wakikwea kilima hatari pembezoni mwa mlima wa Volcano huku moshi mzito ukifuka kutoka kwenye moto wa lava unaotiririka kwenye ardhi, ndio taswira inayowakaribisha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/1GN2z
Kongo Goma Vulkan Nyiragongo
Mlima wa Volkano, NyiragongoPicha: picture alliance/Mary Evans Picture Library/W. Warren

Si hayo tu chini ya mlima huo, utasikia sauti za ngurumo sawa na mawimbi ya bahari kutokana kishindo cha vipande vya mwamba uliopasuka vinavyoruka angani wakati ziwa hilo mojawapo ya lava kubwa duniani na Volcano iliyo hai zaidi ikionesha moja ya maajabu yake.

Bila shaka hilo ndilo linalowapa matumaini wakongo ya eneo hilo kuwavutia watalii zaidi licha ya nchi hiyo kushuhudia migogoro.

Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limekuwa ngome ya vita vya waasi kwa miongo kadhaa lakini vivutio kama hivyo vimesaidia kuwarejesha watalii katika mbuga ya kitaifa ya Virunga ambayo ilifunguliwa tena mwaka jana baada ya mapigano kugeuka na kuwa neema kwake. Msitu unaozunguka milima katika mbuga hiyo ina ukubwa wa kilo mita za mraba elfu 7,800 ni makaazi ya Sokwe wa milimani ambao ni muhimu katika uingizaji wa mapato yanayotokana na utalii hasa ikizingatiwa kwamba wanakabiliwa na hatari ya kutoweka kabisa duniani.

Kilichowaleta watalii

Mmoja wa wahudumu katika mbuga hiyo anasema, vita vilipozuka sokwe hao walitoroka chini ya volkano hadi mjini Goma kilomita 20 kusini baada ya eneo hilo kutekwa na waasi kwa mda mfupi mwaka 2012. Mapigano hayo yaliathiri sekta ya utalii katika sehemu hiyo.

Kwa mujibu wa Afisa mkuu msimamizi wa mbuga hiyo Emmanuel de Merode, vikosi vya waasi bado vinapania kuendesha shughuli katika mbuga ya Virunga.Binafsi De Merode anasema aliwahi kushambuliwa na waasi waliokuwa na bunduki na kujeruhiwa mwaka 2014. Lakini afisa huyo ambaye amepata mafunzo na uwezo wa kutumia silaha kwa ustadi anasema sasa hali ni salama na watalii wanarudi kulitembelea eneo hilo. Watalii wanaotaka kuwaona na kukaa na familia ya sokwe wanatozwa ada ya dolla 400 kwa muda wa saa nzima wakati ada inayotozwa wale wanaotaka kukwea mlima wa Volcano wanatozwa dolla 250.

Kongo Virunga National Park getöteter Gorilla
Mbuga ya kitaifa ya Virunga, DR KongoPicha: Getty Images

Merode anaongezea kuwa mapato yanayotokana na utalii ni muhimu kwa uhai na mustakabali wa mbuga ya Virunga inayowasaidia watu milioni nne ndani na nje ya mbuga hiyo pamoja na kuimarisha amani na maendeleo ya eneo hilo. Utalii pia una mchango mkubwa katika kuwapatia wakaazi kipato kinachotokana na njia mbadala na kujiepusha na ukataji miti kwa ajili ya kuchoma mkaa huku pia ikiwa ni njia inayowatia motisha wa kuilinda mbuga hiyo.

Mnamo mwaka 2011, zaidi ya wageni 3,000 waliitembelea mbuga ya Virunga lakini ghasia zilipelekea mbuga hiyo kufungwa mwaka wa 2012 na tangu wakati huo mbuga hiyo ilifunguliwa tena upya karibu mwisho wa mwaka 2014. Idadi ya watalii kufikia sasa imegonga 3,000 hata kabla ya mwaka huu kukamilika.

Idadi ya watalii yaongezeka

Takriban watalii kumi na sita wanaweza kukwea hadi kilele cha mlima kwa siku. Safari ya karibuni iliwashirikisha watalii wengi kutoka Marekani, Ubelgiji, Uingereza na Isarael. Filamu kwa jina "VIRUNGA" ambayo inaelezea juhudi za kuhifadhi mbuga inayosifika kuwa kongwe zaidi barani afrika dhidi ya vita,wawindaji haramu na makampuni ya mafuta pia imechangia hamu ya watalii kuzuru eneo hilo.

Melanie Gouby mmoja wa waandishi habari za uchunguzi kutoka ufaransa ambaye taarifa yake juu ya njama ya makampuni ya mafuta kunyakua sehemu ya mbuga hiyo iliangaziwa katika filamu ya Virunga anasema nikimnukuu...Kila mtu anayekuja kutembea virunga,kuna matumaini kuwa mambo yatakuwa mazuri. Mwisho wa nukuu.

Guoby anamalizia kwa tabasamu la ufahari kuwa watalii wamerejea tena katika mbuga ya hifadhi ya wanyama ya virunga mda mfupi baada ya mapigano. kubwa zaidi ikiwa ni kutokana na wao kutizama filamu aliyochangia utayarishaji wake.

Giza linapoingia na viwango vya baridi vikipanda hadi kuwa barafu, joto linalotokana mvuke wa kuyeyuka kwa mwamba chini ya volkeno inapasha joto mikono ya watalii huku wakirewesha miguu yao kuelekea chini ya mlima kupata onyesho la kipekee linalowaacha wakihisi kana kwamba wamejionea jinsi ulimwengu ulivyoumbwa nikimnukuu mmoja wa watalii hao

Mwandishi: Ambia Hirsi/Afp

Mhariri:Yusuf Saumu