SUKKUR: Benazir Bhutto atembelea kijiji alikotokea | Habari za Ulimwengu | DW | 27.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SUKKUR: Benazir Bhutto atembelea kijiji alikotokea

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan,Benazir Bhutto amewasili Larkana,wilaya ya kusini ya Sindh, ambako ukoo wa Bhutto una mizizi yake.Akiwa chini ya ulinzi mkali,Bhutto alikwenda kutembelea kaburi la baba yake alieuawa,Zulfiqar Ali Bhutto, ambae pia alikuwa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan.

Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na Bhutto nje ya mji wa Karachi tangu shambulizi la kutaka kumuuawa siku tisa zilizopita,kusababisha vifo vya takriban watu 140.Shambulizi hilo lilifanywa saa chache tu baada ya kuwasili kwake nchini Pakistan baada ya kuishi uhamishoni miaka minane iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com