1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Sudan: al-Burhan aashiria kulikubali pendekezo la IGAD

27 Aprili 2023

Mkuu wa Majeshi ya Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ameashiria kukubali pendekezo la Jumuiya ya Ushirikiano wa Maendeleo ya serikali za nchi za Afrika Mashariki (IGAD) la kuongeza muda wa kusitisha mapigano.

https://p.dw.com/p/4QbtX
Sudan Khartum | Kämpfe zwischen Armee und RSF-Miliz | General Abdel Fattah al-Burhan
Picha: EL TAYEB SIDDIG/REUTERS

Muda huo wa kusitishwa mapigano utaongezwa kwa saa zingine 72 na kuwapeleka wajumbe wa jeshi wa pande zote mbili zinazopingana katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kwa ajili ya mazungumzo.

Soma pia: Mapigano yazuka upya nchini Sudan

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amezungumza na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat juu ya hali ya nchini Sudan. Viongozi hao, pia wamejadili mikakati ya kuyamaliza mapigano ya nchini Sudan.