1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Sudan Kusini kuandaa uchaguzi wa kwanza wa rais 2024

5 Julai 2023

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameahidi kuwa uchaguzi uliocheleweshwa ambao unatarajiwa kufanywa mwaka ujao utaendelea kama ilivyopangwa na kuwa atagombea kiti cha urais.

https://p.dw.com/p/4TQvU
Salva Kiir Mayardit
Rais wa Sudan Kusini Salva KiirPicha: Samir Bol/ZUMAPRESS/picture alliance

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameahidi kuwa uchaguzi uliocheleweshwa ambao unatarajiwa kufanywa mwaka ujao utaendelea kama ilivyopangwa na kuwa atagombea kiti cha urais. Kiir amewaambia wafuasi wa chama chake tawala cha SPLM kuwa anakaribisha idhini yao ya kugombea urais mwaka wa 2024 akiitaja kuwa tukio la kihistoria. Hakuna mgombea mwingine aliyetangaza nia yake lakini mpinzani wake wa kihistoria Riek Machar anatarajiwa kugombea.

Ni wakati wa kuzungumza amaniMnamo Agosti mwaka jana, viongozi hao wawili walirefusha serikali yao ya mpito kwa miaka miwili, wakitaja haja ya kuzishughulikia changamoto zilizozuia utekelezaji wa makubaliano ya amani. Kiir amesema jana kuwa changamoto hizo zitashughulikiwa kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba mwaka ujao. Kiir, kamanda wa vita vya msituni, amekuwa rais pekee wa taifa hilo tanfu alipoliongoza kupata uhuru kutoka kwa Sudan mwaka wa 2011.