1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan: Baraza jipya la mawaziri limeapishwa

Yusra Buwayhid
9 Septemba 2019

Baraza hilo jipya la mawaziri 18 limeapishwa na linaunda serikali ya kwanza nchini  Sudan tangu kuondolewa madarakani kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir.

https://p.dw.com/p/3PGuF
Sudan Premierminister Abdalla Hamdok
Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Kamati ya wanachama 18 nchini Sudan iliapishwa hapo jana Jumapili. Kulingana na shirika la habari la serikali (Suna), hafla hiyo ilifanyika katika ikulu ya Rais mjini Khartoum.

Baraza hilo jipya la mawaziri linaunda serikali ya kwanza nchini  Sudan tangu kuondolewa madarakani kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir. Baraza hilo jipya la mawaziri lina wanawake wanne ikiwa ni pamoja na mwanamke wa kwanza kushikilia wadhfa wa waziri wa mambo ya nchi za nje.

Serikali hiyo mpya imeanzishwa kwenye muktadha wa kugawana madaraka baada ya kufikiwa makubaliano kati baraza la kijeshi na wanaharakati wanaotetea demokrasia nchini Sudan.

Rais wa zamani Omar al Bashiri aliyetawala kwa miaka 30 sasa anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi baada kupatikana kiasi kikubwa cha fedha za kigeni nyumbani kwake.