1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan: Afisa wa UN akamatwa kwa madai ya kumnyanyasa mtoto

29 Novemba 2017

Raia mmoja wa Sudan ambaye ni mfanyakazi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kumnyanyasa kijinsia mtoto mdogo

https://p.dw.com/p/2oRU2
UNAMID-Friedenssoldaten
Picha: ASHRAF SHAZLY/AFP/Getty Images

Raia mmoja wa Sudan ambaye ni mfanyakazi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kumnyanyasa kijinsia mtoto mdogo. Kikosi hicho kimesema kuwa polisi huyo alikamatwa siku ya Jumapili.

Mwathirika wa tukio hilo lililotokea katika eneo la El Fasher pia ni raia wa Sudan. Mkuu wa kikosi hicho, Jeremiah Mamabolo amesema kuwa umoja huo unalaani vikali unyanyasaji wowote wa kijinsia unaofanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Amesema wanaongozwa na sera za kutovumilia matukio ya kuchukiza na hawatovumilia au kukubaliana na matendo kama hayo.

Kutokana na kuwa raia wa Sudan, mtuhumiwa huyo hana kinga kamili inayotumika kwa wafanyakazi wa kigeni katika kikosi hicho. Maafisa wa Sudan wanadai kuwa mzozo katika jimbo la Darfur umekwisha, lakini wataalamu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa mara kwa mara wamekuwa wakiripoti kuhusu visa vya ukiukwaji wa haki, ikiwemo ubakaji katika kambi wanazoishi watu wasio na makaazi.