STOCKHOLM : Mwandishi wa BBC alietekwa Gaza yuko hai | Habari za Ulimwengu | DW | 20.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

STOCKHOLM : Mwandishi wa BBC alietekwa Gaza yuko hai

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesema amepata taarifa za ujasusi zenye kuthibitisha kwamba mwandishi habari alietekwa nyara wa shirika la Utangazaji la Uingereza BBC Alan Johnston yuko hai.

Akizungumza akiwa ziarani mjini Stockholm Abbas amesema alikuwa anajuwa ni kundi gani lililokuwa likimshikilia Johnston lakini hakutowa ufafanuzi.Mwandishi huyo wa habari wa BBC alitekwa kwa mtutu wa bunduki kutoka kwenye gari lake katika mji wa Gaza City zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Mwishoni mwa juma kundi la wanamgambo wa Kiislam lilisilojulikana limedai kwamba limemuuwa Johnston.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com