1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Srilanka -shambulio la bomu lagharimu maisha ya watu 10

Hamidou, Oumilkher6 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dcxg

Colombo:

Watu wasiopungua 10 wameuwawa kufuatia shambulio la bomu nchini Srilanka.Waziri wa usafiri ni miongoni mwa wahanga wa shambulio hilo.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali,bomu hilo limeripuliwa wakati wa hafla moja katika mkoa wa Gampaha.Waziri wa usafiri Jeyaraj FERNANDOPULLE alishiriki katika hafla hiyo,bomu liliporipuliwa na kumuangamizia maisha yake pamoja na ya watu wengine tisaa.Serikali ya Srilanka inawalaumu waasi wa Tamil kua nyuma ya shambulio hilo.Ugonvi katika kisiwa cha srilanka umezidi makali tangu serikali ilipotangaza mwezi January uliopita kuvunja makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyodumu miaka sita .Kabla ya hapo pande hizo mbili zinazohasimiana zilikua kila wakati zikiyaendeya kinyume makubaliano.