1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Srebrenica. Washirika wa Karadzic na Mladic wafungiwa akaunti zao.

22 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpd

Maafisa wa Kiserb nchini Bosnia wamezuwia akaunti za benki za watu 33 wanaotuhumiwa kuwasaidia watuhumiwa wa uhalifu wa kivita ambao wamejificha Radovan Karadzic na Ratko Mladic.

Miongoni mwa walioorodheshwa ni pamoja na rais wa zamani wa Bosnia Mserb Mirko Sarovic na waziri wa ulinzi wa zamani wakati wa vita Bogdan Subotic.

Uamuzi huo ulichukuliwa na mjumbe wa jumuiya ya kimataifa nchini Bosnia , Christian Schwarz-Schilling.

Mahakama ya kimataifa inayowahukumu wahalifu wa kivita katika iliyokuwa Yugoslavia ya zamani inamhitaji Karadzic na Mladic , ambao wanakabiliwa na madai dhidi ya mauaji ya mwaka 1995 ya Waislamu 8,000 wanaume katika eneo la Bosnia lililokuwa katika vita la Srebrenica.

Watu hao wawili wameendelea kuwa mafichoni kwa zaidi ya miaka 11 iliyopita.