Spika wa bunge la Iran alionya shirika la IAEA juu ya Mzozo wa Nuklia | Habari za Ulimwengu | DW | 07.06.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Spika wa bunge la Iran alionya shirika la IAEA juu ya Mzozo wa Nuklia

-

TEHRAN

Spika wa bunge mwenye usemi mkubwa nchini Iran Ali Larijani amelionya shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Nuklia la IAEA juu ya kupoteza wakati katika mzozo unaohusu mpango wa nuklia wa nchi hiyo. Spika huyo ambaye alikuwa mpatanishi mkuu katika suala la Nuklia la Iran amesema nchi yake imekuwa wazi na shirika hilo na sasa linataka kukanganya mambo juu ya mpango huo wa Iran hali ambayo ameonya huenda likaliletea matatizo makubwa shirika hilo. Amesema Iran haina hana ya kulirefusha suala hilo la Nuklia.Wiki hii Iran ilishutumiwa vikali katika mkutano wa shirika hilo la IAEA kwa madai kwamba nchi imeshindwa kuwa wazi juu ya madai ya kuunda silaha za kinuklia.

Ripoti mpya ya mkuu wa shirika la IAEA Moahmmed Alibaraedei imeishutumu Iran kwa kuficha maelezo juu ya madai kwamba inataka kutengeneza silka za Kinuklia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com