Somo la 50 – Kijerumani kama lugha ya kigeni | Radio D Teil 2 | DW | 02.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 50 – Kijerumani kama lugha ya kigeni

Safari hii Jan ametemebelea shule inayotoa mradi maalumu kabisaa wa Kijerumani kwa wanafunzi wake. Anawauliza wanafunzi kwa nini wanajifunza Kijerumani mbali na lugha yao mama, na nini wanataka kukifanya baadae maishani.

Jan anakuja na ripoti kutoka shule ambayo asilimia 80 ya wanafunzi wake ni wahamiaji na kuwatambulisha mradi usio wa kawaida wa Kijerumani. Huko anakutana na Vladmir, Yen-Lin na Gülseren, ambao wanaripoti kuhusu uzoefu wao wa lugha mbili tofauti na ugumu wanaokumbana nao katika kujifunza Kijerumani.
Safari hii profesa anawarahisishia wasikilizaji na kujikita tu katika somo fupi la sarufi.
Anafafanua vifungu vya maneno vyenye kiunganishi cha "bevore", kinachoainisha tukio katika wakati uliopita.

Vilivyopakuliwa