Somo la 47 – Ujenzi wa ukuta | Radio D Teil 2 | DW | 02.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 47 – Ujenzi wa ukuta

Mjini Berlin Paula, Philipp, Jan na Josefine wanatembelea Reichtag, lango la Brandenburg na Mauerweg - au njia ya ukuta, inayoonyesha mahala ulipokuwa ukuta. Redio D inawasilisha mchezo wa redio kuhusu ujenzi wa ukuta.

Jioni ya Agosti 13, 1961, Polisi ya taifa ya Ujerumani Mashariki inaanza kujenga ukuta kwenye mpaka na Berlin Magharibi. Wanandoa wawili ambao nyumba yao inaangaliana moja kwa moja na mpaka wanaamua kutoroka. Upande wa Magharibi kikosi cha zima moto kinasubiri na kuwakamata watu wote wanaoruka kutokea madirishani. Katika somo la leo la sarufi tuna kibainishi kisichodhihirishi cha "ein" na kijina kisichodhihirishi cha "eins". Profesa anavuta usikivu wako kwa changamoto kadhaa ambazo mtu anapaswa kuziangalia katika hali kama hizi.

Vilivyopakuliwa