Somo la 45 – Katika jumba lahisia za mapenzi | Radio D Teil 2 | DW | 02.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 45 – Katika jumba lahisia za mapenzi

Mwishoni mwa muda wao mjini Jena, maripota wawili wanayatembelea makumbusho ya kuvutia hasa. Katika jumba la mapenzi wanakutana na magwiji kadhaa wa kufikiri wa Kijerumani wa karne ya 18.

Jumba la mapenzi mjini Jena limekusanya sanaa na fasihi za kale za mitindo ya hisia za kimapenzi. Hapa wageni wanaweza kujifunza zaidi kuhusu njia mpya za kufikiri za zama hizo na kujifunza kuhusu jaribio la mapinduzi ya kisomi na kishairi. Waandishi hao wawili kutoka Redio D wanawapeleka wasikilizaji katika makumbusho hayo na kuwatambulisha kwa Fitche, Novalis na salon ya Caroline Schlegel. Kukiwa na mengi yanayoendelea wakati mmoja, yumkini ni sawa kwa profesa kufafanua viunganishi vya "als" na "wenn", vinavyoweza kutumiwa kuelezea matukio ya wakati mmoja.

Vilivyopakuliwa