Somo la 44 - Mji wa magwiji wa kufikiri | Radio D Teil 2 | DW | 02.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 44 - Mji wa magwiji wa kufikiri

Mnamo karne ya 18 magwiji kadhaa wa kufikiri walihamia Jena kutoka miji mingine. Miongoni mwao mwandishi mashuhuri Friedrich Schiller. Paula na Philipp wanawasilisha mchezo wa redioni kuhusu mhadhara wake wa kwanza Jena.

Katika kipindi hiki wasikilizaji wanajifunza kidogo kuhusu Schiller na Goethe na wanaweza kuzama katika Jena ya karne ya 18. Hapa ndipo Schiller alipotoa mhadhara wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 29. Zaidi ya wanafunzi 500 walihudhuria tukio hilo. Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wasikilizaji, ililaazimu kutafuta mahala pengine kwa ajili ya mhadhara huo katika dakika za mwisho. Profesa anawarejesha wasikilizaji kutoka wakati uliopita hadi ujao na safari hii anaangalia kitenzi "werden" kinachoashiria tukio la wakati ujao.

Vilivyopakuliwa