Somo la 41 – Msaada kutoka hewani | Radio D Teil 2 | DW | 02.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 41 – Msaada kutoka hewani

Waandishi hao wawili kutoka Redio D wanashindwa kuendelea na uchunguzi wao. Wakiwa kwenye mkwamo, ghafla Eulalia anawasili Jena. Pengine anaweza kuwasaidia Paula na Philipp baadhi ya kazi.

Paula na Philipp wanashindwa kuingia kiwanda cha miwani na jengo lenyewe ni refu sana. Hapo ndipo Eulalia anapoingilia kwa vile anaweza kuangalia kutokea hewani ambako maabara za kiwanda zimewekwa. Na bundi huyo mjanja anafanya ugunduzi wa kuvutia. Lakini hapo linatokea jambo lisilotarajiwa. Profesa pia amechanganyikiwa kabisaa na vurugu zote hizo hivyo katika tukio hilo anachukuwa mfano wa kitenzi rejeshi "konzentrieren". Hii inatoa fursa nzuri ya kuviangalia viwakilishi rejeshi.

Vilivyopakuliwa