Somo la 40 – Nyayo motomoto | Radio D Teil 2 | DW | 02.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 40 – Nyayo motomoto

Philipp na Paula wamepata shuku ya kwanza na wanataka kuangalia ni nini wanafanya wataalamu wa leza katika "mji wa miwani" wa Jena. Na tayari wanalo wazo kuhusu wapi wanaweza kupata baadhi ya taarifa.

Katika kiwanda cha kutengeneza miwani Philipp na Paula wanataka kufuatilia jambo. Mahojiano kiwandani hapo yanapaswa kujibu maswali yao. Lakini msemaji hataki kuwapa taarifa zozote na anawafukuza. Maripota hao wanachunguza kwa njia zao na wanageuka mashahidi wa matukio ya siri. Profesa anaonyesha kuwa muongeaji kuliko msemaji wa kiwanda kwa kushughulikia mazungumzo ya kila siku, hasa maneno yaliyofupishwa katika lugha ya kuzungumza.

Vilivyopakuliwa