Somo la 39 – Ugaidi wa leza Jena | Radio D Teil 2 | DW | 02.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 39 – Ugaidi wa leza Jena

Baada ya kuwasili Jena, Paula na Philipp wanataka kufikia kiini cha mashambulizi ya siri ya leza yanayowaweka roho juu wakaazi wa mji huo. Muda mfupi tu linatokea tukio jengine. Nini kinaendelea?

Njiani kwenda hotelini, maripota hao wa Redio D wanatumia fursa hiyo kumuuliza dereva taxi kuhusu matukio yasiyoelezeka mjini humo. Wanakutana na onyo ya ghafla: Kuna mtu anazunguka akiharibu vioo vya magari kwa kutumia mionzi ya leza. Je, mashambulizi hayo yanahusiana na kongamano la leza linaloendelea hivi sasa mjini Jena? Hali ya sarufi inaonekana kutokuwa na hatari. Profesa anafafanua vihusishi vya "mit", "zu" na "in", ambavyo vinatumia nomino itumikayo kama shamirisho yambwa (dative).

Vilivyopakuliwa