Somo la 35 – Beethoven anacheza Beethoven | Radio D Teil 2 | DW | 01.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 35 – Beethoven anacheza Beethoven

Waandishi hao wawili kutoka Redio D bado wanakuna vichwa kuhusiana na iwapo wanafunzi wa muziki wako sahihi katika mashaka yao. Lakini Eulalia bado yuko hatua moja mbele yao tena. Yeye pia amefanya ugunduzi wa usiku.

Eulalia anawasili ghafla mjini Bonn na anakuja kuwasaidia Paula na Philipp kwa mara nyingine. Tayari amemuona mcheza piano na anajua wapi muziki unatokea. Maripota wa Redio D wanafuata ushauri wa Eulalia na kwenda kufanya mahojiano na "Beethoven mdogo". Lakini je, watafanikiwa kumpata mwanamuzi huyo?
Hata kama Paula na Philipp bado hawajafanikiwa kupata maelezo kuhusu matamasha ya ajabu ya piano, profesa wetu anaweza kutuonyesha namna ya kuanzisha jambo wakati akishughulikia vipengele vya chini.

Vilivyopakuliwa