Somo la 34 – Mashetani katika Jumba la Beethoven | Radio D Teil 2 | DW | 01.09.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 34 – Mashetani katika Jumba la Beethoven

Philip na Paula wanataka kubaini nani anacheza piano vizuri hivyo katika Jumba la Beethoven nyakati za usiku. Katika mkahawa wa mtaani wanagundua mambo ya kuvutia. Je, wamepata kidokezo cha kweli au ni umbea tu?

Baada ya usiku mfupi Paula na Philipp wamekaa mkahawani wanaposikia mazungumzo ya kuvutia. Wanafunzi watatu wa muziki wanaonekana kushuku nani anaweza kuwa anacheza piano usiku. Paula na Philipp wanasikia kuhusu mwanafunzi wa muziki wa ajabu na mwenye kipaji cha kipekee ambaye kila moja anamuita "Beethoven".
Wakati Philipp na Paula wakijiuliza ni nani anacheza piano tamu hivyo katika jumba la Beethoven, profesa wetu anaelekeza muda wake kwenye vifungu vya maswali yasiyo ya moja kwa moja bila kiulizi.

Vilivyopakuliwa