Somo la 30 – Jan Becker | Radio D Teil 2 | DW | 26.08.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 30 – Jan Becker

Katika baa kijijini Grünheide, ghafla anajitokeza kijana anaefuatana na Paula kwenye msitari wa kumalizia mbio hizo kwenye ziwa Möllen. Nini anafahamu mgeni huyo kuhusu shindano hilo na kipi kinamuunganisha na Redio D?

Baada ya Philipp kushindwa kuliwasha gari lake, Jan Becker, kijana aliekutana na Paula kwenye baa kabla, anakuja ghafla kuwasaidia. Wakati Philipp akisalia Grünheide, Paula anaendesha na Jan kuelekea Möllensee. Huko ndiko mashindano hayo yanakopasa kumalizikia. Njiani Paula anajifunza kitu kuhusu mgeni huyu ambacho kiukweli alipaswa kuwa tayari anakijua...
Profesa naye anarejea yaliyopita na kutathmini miundo ya vitenzi visaidizi maalumu "müssen" na "wollen".

Vilivyopakuliwa