Somo la 28 – Trabbi dhidi ya Porsche | Radio D Teil 2 | DW | 26.08.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D Teil 2

Somo la 28 – Trabbi dhidi ya Porsche

Kazi nyingine ya Paula na Philipp inawapeleka katika kijiji kidogo jimboni Brandenburg. Hapa kunafanyika aina maalumu kabisaa ya mashindano. Bila shaka maripota hao wawili wa Redio D wasingekosa tukio hilo.

Shindano lisilo la kawaida limewaleta Paula na Philipp nje ya mji. Awali haikuonekana kama kulikuwa na mengi yanayofanyika hapa. Lakini baada ya kuwasili Grünheide jimboni Brandenburg, wanavutiwa zaidi. Watu zaidi wanamiminika katika baa ya eneo hilo. Dereva wa Trabbi, ambalo ni gari maarufu la Ujerumani Mashariki, anadai gari lake linakimbia kuliko Porsche.
Kwa profesa, shindano hilo ni fursa nzuri ya kuiangalia kwa karibu mifumo ya ulinganishaji vivumishi. Ni gari ipi inakimbia, ipi inakimbia kuliko nyengine, na ipi ina kasi kubwa zaidi kwa ujumla?

Vilivyopakuliwa