1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SOLOMON ISLANDS: Wimbi la Tsunami lavuma kwa kasi

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDJ

Wimbi la tsunami limepita katika ufukwe wa pwani ya visiwa vya Solomon kufuatia tetemeko la ardhi chini ya bahari kusini mwa bahari ya Pacific.

Mawimbi makubwa yalivamia upande wa magharibi wa visiwa vya Solomon mapema leo, kuna ripoti kuwa baadhi ya watu hawajulikani walipo.

Onyo la tsunami limetolewa katika maeneo ya New Papua Guinea, kaskazini mashariki mwa Australia na katika baadhi ya visiwa vya Pacific.

Tetemeko hilo la ardhi lenye viwango vya rishta 8.0 lilikwenda hadi umbali wa kilomita 345 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa visiwa vya Solomon, Honiara ulio kaskazini mashariki mwa Australia.