1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sofia. Chama cha upinzani kuwa na viti vingi bunge la umoja wa Ulaya.

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC00

Matokeo ya mwanzo rasmi katika uchaguzi wa kwanza nchini Bulgaria kuwachagua wabunge wa bunge la Ulaya unaonyesha kuwa chama cha upinzani cha GERB kikiwa kinaongoza.

Chama hicho kimepata asilimia 21.69 ya kura , ikilinganishwa na chama tawala cha Kisoshalist ambacho kina asilimia 21.41.

Chama cha watu wenye asili ya Uturuki cha MRF, chama kilichoko katika serikali ya mseto nchini humo kimepata asilimia 20.26 ya kura.

Vyama hivyo vitatu kila kimoja kinaweza kupata viti vitano kati ya viti 18 vya Bulgaria katika bunge la Ulaya.

Chama cha Nationalist Attack Party kimepata kiasi cha asilimia 14 ya kura na kinaweza kupata kati ya viti viwili na vitatu katika bunge hilo la Ulaya.

Chama cha Kiliberali cha NMS cha mfalme wa zamani Saxe-Coburg, chama cha tatu katika muungano wa serikali , kina asilimia 6.26.

Watu waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 30 ya wapiga kura wote.