Slovenia yakosolewa kwa sheria yake mpya ya wakimbizi wa siasa | Habari za Ulimwengu | DW | 07.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Slovenia yakosolewa kwa sheria yake mpya ya wakimbizi wa siasa

GENEVA:

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi limeikosoa sheria mpya kuhusu ukimbizi ya Slovenia likisema haifikii kiwango cha kimataifa kinachohitajika.Miongoni mwa mengine sheria hiyo inawaweka wale wote wanaomba hifadhi ya kisiasa katika hali ya wasiwasi kwani aidha mkimbizi huyo atafungwa jela ama kurejeshwa kule alikotoka.Slovania ,ambayo imechukua urais wa umoja wa Ulaya januari Mosi, sheria yake hii imeanza kutekelezwa Ijumaa.Sheria hii mpya ilitungwa kwa kulinganana na utaratibu wa wakimbizi

wa Umoja wa Ulaya baada ya nchi hiyo, ambayo zamani ilikuwa mkoa wa Yugoslavia,kujiunga na umoja huo mwaka wa 2005.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com