1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SINGAPORE CITY: Marekani yatoa wito wa msaada zaidi kwa Afghanistan.

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvf

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Robert Gates, amezitaka nchi za bara la Eshia kuipa Afghanistan misaada zaidi na pia kuendeleza ushirikiano wa kieneo kukabiliana na ugaidi.

Waziri huyo wa Ulinzi alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa bara hilo kuhusu usalama.

Robert Gates pia ametahadharisha mataifa hayo kuwa mradi wa Iran wa nishati ya kinyuklia si hatari tu kwa bara la Ulaya bali pia kwa bara la Eshia.

Waziri huyo wa Marekani ameyataka mataifa hayo kuunga mkono vikwazo zaidi dhidi ya Iran ambayo ndiyo njia salama ya kuishinikiza nchi hiyo kusimamisha mradi wake huo.

Waziri Robert Gates aliigusia kidogo China akisema Marekani ina wasiwasi kutokana na tabia ya nchi hiyo kuweka siri, kiasi cha fedha inazotumia kwa shughuli za kijeshi.

Naibu mkuu wa majeshi ya China Luteni Jemedari Zhang Qinsheng amesema serikali yake inaendeleza majeshi yake kwa lengo la kujilinda.