Simba kucheza na APR kwenye kilele cha Simba Day
3 Agosti 2024Matangazo
Leo macho ya wapenda soka nchini Tanzania na Afrika ya Mashariki yatakuwa katika dimba la Benjamini William Mkapa katika kilele cha siku ya Simba Day.Katika tukio hilo la kila mwaka timu ya Simba, moja ya klabu kongwe zaidi za mchezo wa kandanda nchini Tanzania, itakuwa inatambulisha wachezaji na benchi lake la ufundi kwa msimu mpya wa ligi wa mwaka 2024/ 2025
Mapema hii leo mashabiki wa timu hiyo ya Afrika Mashariki walianza shamra shamra kwa mabango yaliyoandikwa msemo wao wa msimu huu wa ´Ubaya Ubwela´ na kuingia uwanjani kusubiri tukio hilo litakalopambwa na burudani ya wasanii mbalimbali wa nchini Tanzania.
Utambulisho huo utahitimishwa kwa mchezo wa kirafiki kati ya Simba na APR ya Rwanda baadaye jioni.