Siku ya kimataifa ya Familia | Masuala ya Jamii | DW | 15.05.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Siku ya kimataifa ya Familia

Leo ni siku ya kimataifa ya Familia.Kauli mbiu ya mwaka huu ni Mama na jamii,jinsi ya kupambana na changamoto katika ulimwengu unaobadilika.

Siku hii ilizinduliwa rasmi mwaka 1989 kwa lengo la kuyapa kipa umbele masuala ya familia na jamii.Katika hotuba yake ya mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alitoa wito wa kuimarisha maisha ya kina mama kwani ndio mlezi wa kizazi kijacho.Malengo ya millennia yameyazingatia masuala ya kina mama kwa kina ila bado hatua zaidi zinahitajika kupigwa.Jee hali visiwani Zanzibar,Tanzania iko vipi?

Hilo ndilo swali Thelma Mwadzaya alilomuuliza Fathiya Zahran Salim naibu mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake katika Baraza la CUF Visiwani Zanzibar.

Mwandishi: Thelma Mwadzaya

Mhariri: Josephat Charo
Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com