1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sierra Leone yapiga mnada almasi ya "Amani"

Sekione Kitojo
5 Desemba 2017

Wakati serikali Afrika zikiwa mara kadhaa zikishutumiwa kwa ufisadi na rushwa, na utajiri mkubwa wa madini katika bara hilo ukiwa hauwanufaishi wananchi, hali huenda ikasimuliwa vingine kutokana na tukio moja muhimu

https://p.dw.com/p/2oo8k
Riesendiamant Koh-i-noor
Picha: Getty Images/AFP

Moja kati  ya  almasi  kubwa  kabisa  duniani  iliuzwa  kwa  kitita  cha  dola milioni 6.8 na  nchi ya  Sierra  Leone  siku  ya  Jumatatu ili kugharamia  miradi  ya  maendeleo  ya  nchi  hiyo, na  kutoa  pigo kubwa  kwa  walanguzi  wa  maliasili  kama  hizo  barani  Afrika.

Almasi  hiyo  iliyokuwa  na  ukubwa  wa  yai la  kuku , yenye  karati 709 iligunduliwa  na  mchungaji  mmoja  wa  kanisa  na  ilifikishwa katika  mnada  mjini  New York  na  Laurence Graff, tajiri  mkubwa bilionea  Muingereza  na muuzaji  wa vito  vya  thamani , kwa  mujibu wa  kundi  la  Rapaport, mtandao  wa  kimataifa  wa  biashara  ya almasi  ambalo  lilihusika  katika  biashara  ya  almasi  hiyo.

Sierra Leone Diamantensuche in Koidu
Wachimbaji wa madini ya Almasi nchini Sierra Leone katika mto wilayani KoiduPicha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Mapato  ya  mauzo  ya  almasi  hiyo  ambayo  ilipewa  jina "Almasi ya  amani,"  serikali  itapata  asilimia  59  ya  mauzo  ama  kiasi  cha dola  milioni  3.9  katika  kodi ili  kuweza  kugharamia  mradi  ya  maji safi, umeme, shule, vituo  vya  afya  na  barabara, amesema  Martin Rapaport wa  kundi  hilo  la  Rapaport.

"Wakati  serikali  katika  bara  la  Afrika , zimekuwa  zikielezwa kutumbukia  katika  rushwa, na  utajiri  wa  madini  hauwafikii wananchi ", amesema  Abdulai Bayraytay , msemaji wa  rais  wa Sierra  Leone  Ernest Bai Koroma, katika  mkutano  na  waandishi habari.

Mauzo  hayo  katika   mnada  yanakuwa  ya  kwanza  kutokana  na almasi  iliyopatikana  nchini  Sierra  Leone yalifanyika  hadharani, na maafisa  wa  serikali  walisema  wanamatumaini  itakuwa  hatua  ya kwanza  mbele  katika  kumaliza biashara  haramu  ya  almasi nchini humo.

Russland eine Handvoll Diamanten
Almasi katika chumba cha maonesho katika kituo cha upembuzi nchini UrusiPicha: picture-alliance/dpa/Y. Smityuk

Almasi zilichochea  vita 

Almasi  zilichochea  vita  vya  wenyewe  kwa  wenyewe  nchini Sierra  Leone  katika  miaka  ya  1990, wakati  wapiganaji  waasi walipowalazimisha  raia  kuchimba  mawe  hayo  ya  thamani  na kununua  silaha  kutokana  na  mapato  ya  mauzo  ya  almasi , na kusababisha  kubatizwa  jina  la  "Almasi za damu".

Umoja  wa  Mataifa  uliondoa  marufuku  iliyowekwa  kwa  mauzo  ya almasi  nje  ya  nchi  hiyo mwaka  2003, lakini  sekta  hiyo  ambayo ni  biashara  ya  mabilioni  ya  dola  bado  imezungukwa  na walanguzi.

Kiasi  kilichobaki  cha   mapato   ya  mauzo  ya  almasi  hiyo kitakwenda  katika  kundi  la  nchi  humo  linaloangalia  miradi  ya maendeleo, mchungaji  huyo  wa  kanisa  na  wachimbaji  wengine ambao  waligundua  almasi  hiyo  na  kuifikisha  serikalini, Rapaport alisema.

"Italeta  ushawishi  kwa  wachimbaji  wengine  nchini  humo," Chifu Paul Ngaba Saquee, mkuu  wa  wilaya  ya  Kono  mashariki  mwa Sierra  Leone, ambako  almasi  hiyo  ilipatikana  mwezi  Machi , aliwaambia  waandisjhi  habari.

"Badala  ya  kupitishwa  katika  vichochoro  ambako  almasi  nyingi zinapatikana , watazifikisha  na  kuweka mezani  mbele  ya  serikali, " alisema  mjini  New York . " Huenda  huu  utakuwa  mwanzo  wa  siku mpya  nchini  Sierra  Leone."

Sierra Leone Sieb für Diamanten
Upembuzi wa madini ya Almasi nchini Sierra LeonePicha: DW/T. Ford

Juhudi  za  kwanza  kuiuza  almasi  hiyo zilishindwa  mwezi  Mei wakati Sierra  Leone  ilipokataa  kiwango  cha  juu  cha  malipo  ya dola  milioni 7.8.

Mara  hii, jiwe  hilo  la  thamani  lilioneshwa  kwa  watu 70  ambao walikuwa  na  uwezo  wa  kulinunua  na maombi  saba yaliwasilishwa, kwa  mujibu  wa  Rapaport.

Mwandishi : Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri : Mohammed  Abdul Rahman