Siasa ya nje ya Ujerumani 2007 | Matukio ya Kisiasa | DW | 20.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Siasa ya nje ya Ujerumani 2007

Kanzela Angela Merkel ana kila sababu ya kujivunia mwaka 2007 katika siasa za nje za Ujerumani na mchango wake.

default

Angela Merkel na Donald Tusk wa poland.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani,ana haki ya kuangalia mwaka huu 2007 au miezi 12 iliopita kwa jicho la mafanikio makubwa katika siasa za nje za Ujerumani.

Mwaka ulianza kwa ziara mjini Washington,Marekani ili kuimarisha usuhuba uliokuwapo tangu zamani na Marekani ,lakini uliregarega chini yaKanzela .Schröder,kanzela wa zamani aliemtangulia.

Pia mwaka umemalizika kwa ziara nyengine kwa George Bush huko Texas.

Kati ya ziara zake za kwanza ni zile katika miji kama Ilulissat na Mazar el-Sharif huko Afghanistan , na kuwa kiongozi wa kwanza kujionea kwa macho yake kuzidi ujoto huko Greenland kunakoyayuka barafu na halafu akavitembelea vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan.

Alifanya pia ziara katika miji mengine kama vile Beirut,nchini Lebanon, Jeruselem na hata Dubai.Ziara hizo zote zimebainisha nia ya Ujerumani ya kuchangia mno zaidi katika utaratibu wa kusaka amanio katika mashariki ya kati.

Ziara zake mjini Cape Town,Afrika Kusini,Monrovia,Liberia huko Afrika magharibi na Addis Ababa,makao makuu ya Umoja wa Afrika, ni ushahidi dhahiori wa kujitolea binafsi bibi Angela Merkel kulisaidia bara la Afrika kujikomboa kwenye shida zake.

Kanzela huyu wa ujerumani alikumbana pia mwaka huu na changamoto kali na viongozi wa Poland mjini Warsaw na hata na warusi huko Sochi na Samara.

Ziara za kawaida kwa majirani wa ujerumani Ulaya ya magharibi wakati ujerumani ilipokalia kiti cha Umoja wa ulaya, m,namo nusu ya kwanza ya mwaka huu zilikuwa ni za desturi tu ukilinganisha na hizo nyengine.

Katuni iliochapishwa ndani ya gazeti la kila siku la BERLIN „TAGESSPIEGEL“ lilisema yote yaliostahiki kusemwa: Bush akikaa bukheri-mustarehe kitini katika nyumba yake ya shambani ya Crwawford anamuuliza , „Vipi,ziara yako ya ujerumani ilikwendaje ?

George Bush nae akachukua msimamo wastani wakutaka maskizano wakati wa ule mkutano wa kilele wa kundi la nchi 8 tajiri-G-8 uliofanyika Heiligendam,Ujerumani hapo juni.

Mwaliko alioutoa kibinafsi Kanzela Meerkel kwa Dalai lama ,kiongozi wa waumini wa madhehebu ya Budha katika afisi yake ya ukanzela mjini Berlin, ulishangiriwa na wakereketwa wa haki za binadamu kwa upande mmoja na wajerumani wengi,lakini ghadhabu kutoka Beijing ilioamua kuvunja mikutano kadhaa ya hadhi ya juu na viongozi wa Ujerumani.

Sasa Kanzela huyu kutoka chama cha wahafidhina cha CDU anaepitisha wakati huu akitamba katika wadhifa wake hadi uchaguzi ujao anatumai atajikingia kura za kutosha hapo 2009 kutawala bila ya mshirika wake wa sasa chama cha waziri wa nje aliempiku Walter Steinmeier.

Uchaguzi huo lakini upo mbali mno.hali ya uchumi ya Ujerumani hainawiri hivyo na chama cha SPD mshirika wake serikalini kimeanza kujiwinda mrengo wa shoto ili kuweza kuitumia vilivyo hali inayoongezeka ya kutoridhika mambo kuanza kwenda mrama.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com