Siasa na jamii | Noa Bongo | DW | 19.10.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Noa Bongo

Siasa na jamii

Siasa hutekeleza wajibu muhimu katika maisha ya kila siku. Kupitia mchanganyiko wa mada mbalimbali zilizozungumziwa katika vipindi hivi, Noa Bongo inakupa sura halisi ya jinsi siasa zinavyoendeshwa barani Afrika.

default

Watu wengi wanadai kuwa kinachohitajika zaidi barani Afrika ni utawala bora - viongozi wa kisiasa wanaotumia mamlaka yao kupigana na umaskini na kubuni mazingira bora na amani kwa minajili ya maendeleo ya bara hili.

Msingi wa elimu kwa viongozi wa kesho wa kisiasa

Vipindi hivi viliangazia mabadiliko na maono ya viongozi kwa bara hili la Afrika katika siku zijazo. Vinachunguza kwa ndani historia ya bara hili na iwapo kuna mafunzo yoyote na pia jinsi ya kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa sasa. Vipindi vinaeleza wazi haki za raia wa Afrika - na jinsi zinavyokiukwa kila siku.

Kupitia vipindi hivi uliweza kufuata nyayo za wahamiaji kutoka barani Afrika na ndoto ya kuishi maisha bora barani Ulaya kupitia mada inayogusia suala nyeti la uhamiaji. Katika vipindi vyote kuhusu masuala ya siasa na jamii Noa Bongo inakusudia kukupa taswira ya viongozi wa siku zijazo, na elimu unayohitaji kuhusiana na suala la uhuru wa kutoa maoni.

DW inapendekeza