MigogoroMali
Mali: Shule zafungwa kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta
27 Oktoba 2025
Matangazo
Uhaba huo umesababishwa na vizuizi vilivyowekwa na wanamgambo wenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda. Mapema mwezi Septemba, wanamgambo wa Jama'at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM) walitangaza kuzuia uagizaji wa mafuta katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi isiyo na bandari, na tangu wakati huo wamekuwa wakishambulia misafara ya malori ya mafuta yanayojaribu kuingia nchini humo.
Hatua hii inatajwa na wachambuzi kuwa ni sehemu ya kampeni ya makundi hayo ya wanamgambo na inayolenga kuzidisha shinikizo kwa serikali ya kijeshi ya Mali kwa kuzuia chanzo kikuu cha uchumi nchini humo.