Sheria mpya kwa wahamiaji nchini Ujerumani | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 19.10.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Sheria mpya kwa wahamiaji nchini Ujerumani

Wahamiaji nchini Ujerumani watalazimika kusoma Kijerumani

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa na kundi la vijana kutoka familia za wahamiaji nchini Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa na kundi la vijana kutoka familia za wahamiaji nchini Ujerumani.

Serikali ya kansela Angela Merkel inatayarisha sheria mpya ambayo itawataka wahamiaji kujijumuisha vizuri zaidi katika jamii ya Ujerumani. Msemaji wa serikali amesema mjini Berlin jana kuwa mapendekezo hayo ni pamoja na ulazima wa kusoma lugha ya Kijerumani na mtu anaweza kuadhibiwa ,iwapo atashindwa kumaliza masomo yanayotakiwa kwa ajili ya kujumuishwa. Matokeo kwa mtu atakayeshindwa inaweza kuwa pamoja na kupunguziwa mafao ya kijamii ama kubatilisha ruhsa ya kuishi nchini. Hata hivyo , muswada huo , ambao unatarajiwa kupigiwa kura mwezi Desemba , pia utaimarisha hatua ya kutambua shahada zilizopatikana kutoka mataifa ya kigeni. Kiasi cha wahamiaji wanaokadiriwa kufikia 300,000 wanaoishi nchini Ujerumani kwa hivi sasa wanashindwa kufanyakazi walizojifunza kwasababu masomo waliojifunza hayajathibitishwa na maafisa wa Ujerumani.

 • Tarehe 19.10.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PhFr
 • Tarehe 19.10.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PhFr
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com