1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sherehe za miaka 17 ya Muungano wa Ujerumani

Oummilkheir3 Oktoba 2007

Ujenzi wa eneo la mashariki ndo kipa umbele cha serikali kuu

https://p.dw.com/p/CB0l
Viongozi wa serikali wakusanyika schwerin kuadhimisha miaka 17 ya muungano
Viongozi wa serikali wakusanyika schwerin kuadhimisha miaka 17 ya muunganoPicha: AP

Spika wa baraza la wawakilishi wa majimbo Bundesrat,waziri mkuu wa jimbo la Mecklenburg Vorpommern,HARALD RINGSTOFF akihutubia sherehe rasmi za kuadhimisha siku kuu ya muungano wa ujerumani hii leo mjini Schwerin amezungumzia umuhimu wa demokrasia huru.

Waziri mkuu wa jimbo la Mecklenburg Vorpommen,jimbo linaloandaa sherehe za muungano wa Ujerumani kwa mara ya pili mwaka huu,baada ya mwaka 1992,Harald Ringstoff amesisitiza umuhimu wa kupigania demokrasi na uhuru.Amesema miaka 17 iliyopita,Ujerumani mashariki pia ilipigania uhuru na demokrasia.manufaa ya mapambano hayo anasema yanaangaliwa hii leo kama jambo la kawaida,lakini anasisiotiza,kuna umuhimu wa kila wakati kushadidiwa:

“Tunabidi tupania kikamilifu dhidi ya visa visivyothamini uhuru,sheria wala murwa na hadhi ya binaadam.Naiwe siasa kali za mrengo wa kulia,hisia za chuki dhidi ya wageni,matumizi ya nguvu shuleni,tunabidi kupaza sauti na kusema kinaga ubaga,kokote kule tuliko-la.”Anasema waziri mkuu huyo.

Raisi wa shirikisho Horst Köhler,kansela Angela Merkel na viongozi kadhaa wa serikali kuu na serikali za majimbo pamoja na wakala za kimataifa zinazowakilishwa mjini Berlin wamehudhuria sherehe hiyo rasmi katika ukumbi wa jingo la michezo ya kuigiza mjini Schwerin.

Akihutubia hafla hiyo kuadhimisha miaka 17 ya muungano wa Ujerumani,kansela Angela Merkel amesema ujenzi wa maeneo ya mashariki unasalia kua kipa umbele cha siasa za serikali yake.

Kansela Angela Merkel amesema bado kuna mengi ya kufanya,licha ya mafanikio yaliyoweza kupatikana.

Miaka kumi na sabaa baada ya muungano pengo upande wa mishahara,ukosefu ajira,na miundo mbinu bado lingalipo kati ya sehemu ya magharibi na ile ya Ujerumani mashariki ya zamani.

Spika wa bunge la shirikisho Nobert Lammert amezungumzia umuhimu wa kujengwa “kitambulisho cha uhuru na muungano” nchini Ujerumani.

“Hadi tutakapokamilisha miaka 25 ya kuporomoka ukuta na kuungana upya,kumbusho kama hilo lazma liwe limeshajengwa,amesema bwana Nobert Lammert katika sherehe za muungano hii leo mjini Schwerin.

Sherehe rasmi zimeanza leo asubuhi kwa misa iliyofanyika katika kanisa kuu la Schwerin,mji mkuu wa jimbo la Mecklenburg Vorpommern,jimbo linalokabiliwa na kishindo kikubwa cha ukosefu wa ajira na ambako chama cha siasa kali za mrengo wa kulia NPD kinawakilishwa katika bunge la jimbo hilo.

Baadae leo usiku rais wa shirikisho Horst Köhler atawapokea katika kasri lake wawakilishi wa kisiasa na kiuchumi kuadhimisha siku kuu ya muungano.

Wakati huo huo mjini Berlin sanamu la kansela wa zamani Helmut Kohl limezinduliwa kutukuza mchango aliyotoa katika kufanikisha muungano wa Ujerumani.