Shelane Flanagan aweka historia NYC Marathon | Michezo | DW | 06.11.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Shelane Flanagan aweka historia NYC Marathon

Mwanariadha wa Marekani Shalane Flanagan amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani kushinda mbio za New York Marathon katika kipindi cha miaka 40

Mkenya Mary Keitany alimaliza katika nafasi ya pili kwa muda wa saa mbili mbili dakika 27 sekunde 54 huku Mamitu Daska wa Ethiopia akimaliza katika nafasi ya tatu.

Flanagan, mwenye umri wa miaka 36, mshindi wa medali ya fedha katika mbio za mita 10,000 kwenye mashindano ya Olimpiki ya Beijing mwaka wa 2008, alimaliza wa pili katika mbio za New York marathon mwaka wa 2010

Kwa upande wa wanaume, Mkenya Geoffrey Kamworor alishinda mbio zake kuu za marathon kwa mara ya kwanza. Kamworor alitumia muda wa saa mbili dakika kumi sekunde 53. Alimpiku Mkenya mwenzake na aliyekuwa bingwa wa rekodi ya dunia Wilson Kipsang aliyemaliza katika muda wa saa mbili dakika kumi sekunde 56 na Muethiopia Lelisa Desisa.

Mbio hizo zilifanika siku chache tu baada ya shambulizi la kigaidi mjini humo kusababisha vifo vya watu wanane na polisi ikaahidi kuimarisha usalama kwa ajili ya mashindano hayo yanayowavutia maelfu ya watazamaji pamoja na wanariadha. Bill de Blasio ni Meya wa New York

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman