Sheikh Salman kugombea urais wa FIFA | Michezo | DW | 26.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Sheikh Salman kugombea urais wa FIFA

Sheikh Salman, mwenyekiti wa shirikisho la kabumbu barani Asia amejiunga na orodha ya wagombea wengine watano waliojitokeza hadi sasa kupigania wadhifa wa zrais wa FIFA

Upande wa wagombea wazito wazito anakutikana Michel Platini, aliyesitishiwa kwa muda shughuli zake na Tokyo Sexwale wa Afrika Kusini. Wengine watatu waliosalia wanaonekana kana kwamba hawana nafasi kubwa ya kufanikiwa.

Bado kuna muda lakini hadi saa sita za usiku wa leo kuamkia kesho Jumanne,wakati daftari la maombi litakapofungwa.Orodha ya wanaoomba kugombea wadhifa huo inaweza kuwa ndefu hadi wakati huo na matokeo ya uchaguzi wa atakaemrithi Blatter, February 26 mwakani, hayakadiriki.Mbali na wagombea hao watatu tuliowataja,wengine ni pamoja na Mwanamfalme Ali wa Jordan,Jérome Champagne wa ufaransa na David Nakhid wa Trinidad.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/SID
Mhariri: Gakuba Daniel