1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHARM EL-SHEIKH:Viongozi wa Marekani kutoa msukumo katika mpango wa amani mashariki ya Kati

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdN

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Condoleeza Rice na waziri wa Ulinzi Robert Gates wako eneo la Mashariki ya Kati kushawishi mataifa ya Kiarabu kutia juhudi zaidi ili kuimarisha hali ya usalama nchini Iraq vilevile kudhibiti juhudi za Iran za kuimarisha mpango wake wa nuklia.Viongozi hao wanaoandamana wako mjini Sharm el Sheikh na kutoa ahadi za mabilioni ya dola za msaada wa kijeshi ili kupambana na Al Qaeda,wapiganaji wa Hezbolla,Syria na Iran.Bwana Gates na Bi Rice wanatarajiwa kuzuru nchi ya Saudia na kutoa wito kwa mataifa jirani ya Kiarabu kuunga mkono juhudi za maridhiano kati ya makundi yanayozozana nchini Iraq.

Marekani imejaribu kupata msaada wa mataifa ya Kiarabu kutafuta ufumbuzi wa tatizo la Iraq japo nchi jirani hazina usemi wowote.Saudia ina ushawishi katika viongozi wa kitamaduni wa kiSunni hukui Marekani ikiitaka nchi hiyo kudhibiti mipaka yake ili kuwazuia wapiganaji wanaoegemea upande wa kundi la Al Qaeda kuingia Iraq na kusababisha ghasia.

Iran kwa upande wake inakosoa ahadi ya kuyauzuia silaha mataifa ya Kiarabu yaliyo rafiki na Marekani na kuilaumu Marekani kwa kusambaza hofu na kutoaminiana katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa serikali ya Marekani ujumbe huo wa mawaziri wake unalenga kuashiria kujitolea kwake kutafuta suluhu katika eneo la Mashariki ya Kati.