1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SHARM EL SHEIKH:Mkutano wa kimataifa juu ya Iraq waanza leo Misri

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5F

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice yupo kwenye eneo la Sharm El Sheikh nchini Misri kwa ajili ya mkutano wa siku mbili wa kimataifa kuhusu Iraq.

Wanadiplomasia wengine kutoka nchi za kiarabu,China,Urussi,na Umoja wa Ulaya pia watahudhuria mkutano huo. Hapo jana bibi Rice alikutana na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon na waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki.

Hata hivyo mkutano huo unaolenga kujadili njia za kuisaidia Irak kukabiliana na mashambulio ya waasi huenda ukagubikwa na mazungumzo kati ya Iran na Marekani.

Marekani inaishutumu Iran kwa kuchochea ghasia nchini Iraq na Iran inayapinga madai hayo.