1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la kujitolea muhanga limeua hadi watu 27 Pakistan

16 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D8Zg

ISLAMABAD:

Si chini ya watu 27 wameuawa nchini Pakistan katika mripuko mkubwa uliotokea katika mkutano wa chama cha kiongozi wa upinzani alieuawa Benazir Bhutto.Vile vile takriban watu 100 wamejeruhiwa.Shambulio hilo la kujitolea muhanga limefanywa katika ofisi ya mgombea uchaguzi,Riaz Shah,katika kanda ya machafuko ya kikabila,karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan.

Bhutto binafsi,aliuawa katika shambulizi la kujitolea muhanga mjini Rawalpindi Desemba 27.Mauaji hayo yalisababisha machafuko makubwa nchini Pakistan na uchaguzi ukaahirishwa kwa majuma sita.Wimbi la mashambulizi ya bomu na ya kujitolea muhanga,ni hali inayoshuhudiwa nchini humo kabla ya uchaguzi wa Jumatatu ijayo.