1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la kisu laua watu 5, makao makuu ya polisi Paris

John Juma
3 Oktoba 2019

Polisi wanne wameuawa katika makao makuu ya polisi mjini Paris baada ya mfanyakazi mmoja katika makao hayo, aliyekuwa na kisu kuwashambulia polisi.

https://p.dw.com/p/3Qgxj
Frankreich | Polizei | Messerangriff
Picha: Reuters/P. Wojazer

Maafisa wanne wa polisi wameuawa ndani ya makao makuu ya polisi mjini Paris, Ufaransa baada ya mfanyakazi mmoja aliyekuwa na kisu kushambulia makao hayo.

Inaarifiwa kuwa mshambuliaji huyo pia ameuawa. Rais Emmanuel Macron amelizuru eneo hilo la shambulizi. Sababu ya shambulizi hilo bado haijajulikana.

Idadi ya waliojeruhiwa pia haikujulikana moja kwa moja.

Kiongozi wa chama cha polisi Jean-Marc Bailleul ameelezea kisa hicho kuwa cha uhalifu na si kitendo cha ugaidi.

Eneo hilo la mkasa, lilizingirwa kwa sababu za kiusalama.