1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Limetokea katika kituo cha ukaguzi

17 Januari 2017

Polisi wanne wameuawa na wengine kujeruhiwa nchini Misri katika shambulio la risasi katika kituo cha ukaguzi

https://p.dw.com/p/2VvSt
Ägypten Kairo Polizei Symbolbild
Picha: Reuters/M.A.El Ghany

Shambulizi lililofanywa katika kituo cha ukaguzi kusini magharibi mwa Misri limewaua kiasi ya polisi wanane na kuwajeruhi wengine watatu. Vyombo vya serikali ya Misri vimesema  shambulizi hilo la risasi limefanyika katika jimbo la el-Wadi el-Gedid kilomita 600 kusini magharibi mwa Cairo. Televisheni ya serikali nchini humo imeripoti kuwa shambulizi hilo lilifanyika jana  saa mbili na robo usiku katika kizuizi cha Naqb. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo ingawa kundi la itikadi kalila Dola la Kiisilamu IS limekuwa likidai kuhusika  na mashambulizi ya aina hiyo ikiwa ni pamoja na shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa katika gari , Januari 9, lililofanyika katika kituo cha ukaguzi cha polisi ambapo watu wanane waliuawa.