1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la bomu lauwa watu mjini Baghdad nchini Irak

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD49

Bomu limeripuka magharibi mwa mji mkuu wa Irak Baghdad na kuwauwa watu 10 na wanne wamejeruhiwa. Kabla ya tukio hilo, wanajeshi wa serikali wakishirikiana na wanajeshi kutoka Marekani, wamewauwa watu 11 wakati wa mapigano na watu waliokuwa na silaha katika mji wa Diwaniyah, kusini mwa nchi. Msemaji moja wa kijeshi amesema baadhi ya magengi hayo yalivalia sare za polisi.

Kwa upande mwingine, polisi wamegundua maiti za watu 60 waliouawa baada ya kuteswa, zikiwa ni dalili kwamba walikuwa wahanga wa machafuko ya kidini yanayoendelea kuisibu nchi hiyo.

Na habari zaidi kuhusu Irak, ni kwamba rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein, amefukuzwa tena kutoka mahakamani baada ya mabishano na jaji wa mahakama kuhusu kesi ya mauaji ya kuangamiza jamii inayomkabili.