1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shabiki wa Deportivo auawa kufuatia vurugu

1 Desemba 2014

Kifo cha shabiki wa Deportivo La Coruna katika makabiliano baina ya makundi ya itikadi kali kabla ya mchuano dhidi ya Atletico Madrid, kimezusha miito ya kuchukuliwa hatua dhidi ya “ushabiki wa itikadi kali”.

https://p.dw.com/p/1DxgZ
Madrid Fußball Ausschreitungen Deportivo Coruna gegen Atletico Madrid Spanien
Picha: Reuters/Susana Vera

Tume ya serikali ya Uhispania ya kupambana na machafuko ilikutana leo kujadili matukio hayo ya jana. Francisco Javier Romero Taboada aliyekuwa na umri wa miaka 43, aliokolewa kutoka mto Manzanares karibu na uwanja wa Atletico wa Vicente Calderon na akapatwa na mshutuko wa moyo, kuganda damu mwilini kutokana na maji ya barafu, na majeraha ya kichwa.

Vurugu zilianza karibu saa tatu asubuhi katika kile kilichoonekana kuwa ni makabiliano ya barabarani yaliyopangwa baina ya mashabiki wenye misimamo mikali wa klabu ya Atletico, Deportivo na vilabu vya mjini Madrid, Rayo Vallecano na Alcorcon.

Madrid Fußball Ausschreitungen Deportivo Coruna gegen Atletico Madrid Spanien
Licha ya ghasia zilizotokea, mechi Kati ya Atletico na Deportivo iliruhusiwa kuendeleaPicha: Reuters/Susana Vera

Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo alilaani vurugu hizo baada ya mchuano kukamilika. "Hii ni fursa ya kulaani matukio yaliyotokea karibu kilomita 500 au 1,000 kutoka uwanja wa Vicente Calderon. Nataka kusema kuwa hii haihusu kandanda. Haya ni makundi ya itikadi kali ambayo hukutana na kusababisha vurugu. Marais wa Deportivo La Coruna na Atletico Madrid wanataka kusema wazi kuwa hawahusiki kwa vyovyote na matukio hayo. Kawaida tunatoa wito wa amani na utulivu katika mechi zote" Makundi hayo, ambayo huwa na misimamo mikali ya kisiasa ya mrengo wa kulia, kwa muda mrefu yamekuwa sehemu ya jamii ya kandanda la Uhispania na vilabu vingi vikuu huwayashughulikia katika viwango tofauti vya ustahimili. Diego Godin, ni mchezaji wa Atletico

Kando na tukio hilo, Atletico iliizaba Deportivo mabao mawili kwa sifuri. Katika mchuano mwingine Barcelona ilipata ushindi wa dakika za mwisho mwisho kabisa wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Valencia. Ushindi huo umelipunguza pengo baina yao na viongozi Real Madrid hadi points mbili. Madrid waliweka rekodi mpya ya klabu kushinda mechi 16 mfululizo katika mashindano yote wakati walipowazaba Malaga mabao mawili kwa moja.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Josephat Charo