Serikali ya Umoja wa Komoro na suala la kisiwa cha Anjouan | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Serikali ya Umoja wa Komoro na suala la kisiwa cha Anjouan

Wakati serikali ya Umoja wa Komoro inayoongozwa na Rais Ahmed Abdalla Sambi ikiwa mbioni kulitatua suala la Kisiwa cha Anjouan, raia kadhaa wa Kisiwa hicho wanaoishi katika visiwa vya Ngazija na Moheli wameunda serikali ya uhamishoni itakayowakilisha kisiwa cha Anjouan.

Kuundwa Serikali hiyo kutazidi kuleta utata mkubwa kati ya Serikali ya Umoja na utawala wa Anjouan. Serikali ya Komoro, kupitia waziri wa mambo ya kigeni, imepinga vikali kuwepo kwa Serikali hiyo.

Abdulrahman Baramia anaripoti kutoka Moroni.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com