1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Ujerumani yakanusha ripoti ya Bild an Sonntag kuhusu kupatiwa mafunzo vikosi vya usalama vya Libya

Hamidou, Oumilkher6 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dcxe

Berlin:

Kwa mujibu wa duru za kuaminika za kibalozi,hakuna mafungamano yoyote kati ya kisa cha kupatiwa mafunzo vikosi vya usalama vya Libya na askari polisi wa ujerumani na msaada wa libya katika kuachiliwa huru mahabusi wa visiwani Philippines.Maafisa wa serikali mjini Berlin wamezisuta ripoti kuhusu mafungamano hayo.Gazeti la Bild am Sonntag liliripoti juu ya "mafunzo kinyume na sheria yaliyotolewa na polisi wa Ujerumani kama sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa kuhusu msaada wa Libya katika kuokolewa mahabusi ikiwemo familia ya Wallert ya kutoka Ujerumani.Gazeti hilo limenukuu duru za idara ya upelelezi.Familia Wallert na mtoto wao wa kiume walitekwa nyara mwaka 2000 nawaasi wa kiislam na kushikiliwa mateka kwa miezi kadhaa visiwani Philippines.Libya inasemekana ililipa dala milioni 21 ili waachiliwe huru.Wakati huo huo wizara ya mambo ya nchi za nje mjini Berlin imekanusha ripoti ya jarida la der Spiegel inayodai ubalozi wa Ujerumani mjini Tripoli uliarifiwa kuhusu mafunzo hayo.Wabunge kutoka serikali ya muungano na upande wa upinzani wameshauri kisa hicho kifafanuliwe haraka na ichunguzwe pia kama idara ya upelelezi ilihusika au la.