1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Serbia yavunjwa

11 Machi 2008

Waziri Mkuu wa Serbia Vojislav Kostunica ameivunja rasmi serikali yake.

https://p.dw.com/p/DMMd

BELGRADE

Uamuzi huo umechulukiwa baada ya kikako kifupi cha baraza la mawaziri mjini Belgarde.Kostunica amesema hapo Jumamosi kwamba sababu ya kuvunjika kwa serikali hiyo ni kuwepo kwa tafauti kubwa ndani ya serikali hiyo ya mseto juu ya suala la iwapo nchi hiyo ijiunge na Umoja wa Ulaya.

Rais Boris Tadic lazima sasa avunje bunge na kuitisha uchaguzi mpya yumkini hapo mwezi wa Mei.

Uchaguzi huo unatrajiwa kuwa wa mchuano mkali kati ya Wanademokrasia wa Tadic wanaounga mkono kujiunga na Umoja wa Ulaya na wanasiasa wa msimamo mkali wa kitaifa ambao wanapinga kujiunga na umoja huo venginevyo Umoja wa Ulaya unakataa kujitenga kwa jimbo la Kosovo.